Kilele cha Jubilei ya miaka 50 ya uinjilishaji
Tarehe 5 Julai 2026 parokia iliadhimisha kilele cha Jubilei: vijana 155 walipokea Kipaimara na wanandoa 21 walifunga ndoa.
Dominika tarehe 5 Julai 2026, Parokia ya Mwenyeheri Maria Theresa Ledochowska iliadhimisha kilele cha Jubilei ya miaka 50 ya uinjilishaji (1973–2026).
Kaulimbiu ilikuwa: Jubilei miaka 50 Kiwanja cha Ndege, tunaendelea kukaza mwendo katika Kristo. Misa iliongozwa na Askofu Mkuu Beatus Kinyaiya. Vijana 155 waliimarishwa kwa Kipaimara, na waamini 21 walifunga Ndoa Takatifu.

