Jimbo Kuu Katoliki la Dodoma+255 742 472 725 / +255 783 472 725

← Tangazo

Tangazo

MATANGAZO YA DOMINIKA YA 30 YA MWAKA ‘A’ – 25/10/2026

25 Oktoba 2026

Matangazo ya 25/10/2026

  1. Waamini mnatangaziwa kuwa tutakuwa na usiku wa vijana tarehe 05/12/2026. Gharama ya kushiriki ni Tsh. 80,000/= kwa wanandoa (couple). Pia vijana na wagane wote wanakaribishwa kushiriki kwa gharama ya Tsh. 40,000/=. Tukio litafanyika katika Semina na Clinic ya Ndoa kwa tarehe na ratiba itakayatangazwa hapo baadaye.

  2. Uchaguzi wa kujaza nafasi zilizo wazi katika Jumuiya na Vyama vya Kitume ngazi ya Parokia utafanyika tarehe 07/11/2026. Viongozi watakaochaguliwa watapishwa tarehe 15/11/2026.

  3. Kamati Tendaji ya Uwaka Parokia inawatangazia wanauwaka kuwa watakuwa na semina kila Jumamosi ya pili ya kila mwezi, na Ibada ya Misa Takatifu kuanzia saa 3:00 asubuhi hapa Parokiani. Mseminishaji na muadhimishaji wa Misa ni Paroko.

  4. Tarehe 31/10/2026 wanauwaka watapeleka majitoleo yao kwa Waseminari huko Miyuji. Wanauwaka wote tutakutana Parokiani saa 2:00 asubuhi kwa ajili ya safari.

  5. Wazee na Wastaafu waliopokelewa katika Shirika la Wazee na Wastaafu tarehe 21/10/2026, mnaombwa kukutana leo mara baada ya Misa ya Kwanza, ya Pili na Misa ya Tatu karibu na Sanamu ya Moyo Mtakatifu wa Yesu.

  6. Shirika la Masista wa Ivrea wanawatangazia wazazi na walezi nafasi za masomo kwa mwaka 2027. Huduma zinazotolewa hapa ni: malezi ya watoto wadogo (Day Care) miezi 6 hadi miaka 2; darasa la awali (Nursery School) kuanzia miaka 3; na Shule ya Msingi, darasa la kwanza (Primary), kuanzia miaka 5. Fomu zinapatikana shuleni kwa Masista wa Ivrea.

  7. Wagane, vijana na walei pweke wanaopenda kushiriki semina itakayoandaliwa na Parokia wanaombwa kujiandikisha kwa Makatibu wa Jumuiya za Kibaba kufikia tarehe 31/10/2026. Makatibu wa Jumuiya wawasilishe orodha ya waliojiandikisha kwa mratibu wa H/Walei ifikapo tarehe 31/10/2026.

  8. Viongozi wote wa Jumuiya na Vyama vya Kitume ngazi ya Parokia wanatangaziwa kuwa kutakuwa na semina ya Uongozi Jumamosi tarehe 14/11/2026 kuanzia saa 3:30 asubuhi. Wahusika wote mnahimizwa kushiriki bila kukosa.

  9. Leo Viwawa Kanda ya Yeriko watakuwa na uzinduzi wa filamu ya Mwenyeheri Maria Teresa Ledochowska. Uzinduzi utafanyika saa 11:00 jioni hapa Parokiani katika ukumbi wa Inyasi. Waamini wote mnakaribishwa kuunga mkono.

  10. Tunawashukuru Jumuiya ya Mt. Andrea Kagawa na Mt. Nicholaus Owen kwa kazi nzuri ya usafi na kusimamia utaratibu wa Ibada. Wiki hii ni zamu ya Jumuiya ya Mt. Bernadetha na Mt. Petro Mtume, ambao wataanza zamu siku ya Jumatano na kumaliza Jumapili baada ya kuhesabu sadaka. Wajumbe wa Jumuiya ya Mt. Simoni Zelote na Mt. Yuda Thadei.